2 Nyakati 9 SWHULB
2 Nyakati Chapter 9 SWHULB Bible Verse Images
Copyright © 2019 Door43 World Missions Community
Language: Kiswahili (Swahili)
Translation by: Door43 World Missions Community
Contributors: Alfred Danjuma, Bariki Malisa, Christina Abraham Kileo, Cloud Roman, Daniel Marura Chacha, Dina Mast, Dina Roman, Donald Shadarck Dutuyi, Emmanuel Masanja Mbaaga, Emmanuel Nyamalya, Erasmus Peter Malelo, Ev. Lazaro Chalomhola, Ezekiel Manala, Fred, Gabriel Gidale Merus, Gabriel Lwitakubi Mazige, James Makula, James Semnkai, Jeremiah Masasi, Jesse Katabi Masolwa, John Ojasi, Joyce Gilbert Masasi, Karen Riecks, Kazwanomo, Kennedy, Ker, Lameck Yakobo Tobotobo, Laurent Petro Malelo, Lazarus David Chalomhola, Makene Mafwele, Marco Luma Mahushi, Mathew Nkusa, Mathias William, Mr. James Semnkai .It., Musa Isaya Majama, Musa Luzali, Pastor John Kerim, Pastor Jordan, Philipo Mussa Kanwelle, Raphael Musa, Rev. Charles Mabisa, Rev. Yohana Batano, Robert Ndalahwa, Sadiki Kulwa, Samson Nungwana, Thobias Kazwanomo, Yohana Dutuyi, Yohana Magera, Zelote Loilang'akaki Lukumay, Rev. Erasmus Peter Malelo, Ev. Mathew Kazimoto, Rev. Dr. David Magoke, Rev. Elias Ndema, Rev. Alex Nyuri, Rev. Gungutu Elias, Rev. Lameck Tobotobo, Rev. Catherin D. Matia, Rev. Yohana S Dutuyi, Rev. Donald Dutuyi, GS. Andrew Gewe, Ev. Ezekiel Daudi, Rev. John Ndaluka, Ev. Moses Malugu, Rev. Moses Eliakim Ndege, Past. Isack A. Gomugo, Past. Mathias William, Rev. Yekonia M. Koko, Rev. Elisande Mhanga, Ev. James A. Makula.
This translation is made available to you under the terms of the Creative Commons Attribution Share-Alike license 4.0.
You have permission to share and redistribute this Bible translation in any format and to make reasonable revisions and adaptations of this translation, provided that:
- You include the above copyright and source information.
- If you make any changes to the text, you must indicate that you did so in a way that makes it clear that the original licensor is not necessarily endorsing your changes.
- If you redistribute this text, you must distribute your contributions under the same license as the original.
Credits: In addition, we would like to give very special thanks to eBible.org for making Swahili Unlocked Literal Bible available in MySQL format.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Malikia wa Sheba aliposikia kuhusu umaarufu wa Selemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Akaja pamoja na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliosheheni manukato, dhahabu nyingi, na vito vingi vya thamani. Alipofika kwa
Square Portrait Landscape 4K UHD
Selemani, akamwambia yaliyokuwa moyoni mwake. Selemani akamjibu maswaali yake yote; hakuna kitu kilichokuwa kigumu sana kwa Selemani; hakuna swali ambalo hakulijibu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Malikia wa Sheba alipoiona hekima ya Selemani na ikulu aliyokuwa amejenga,
Square Portrait Landscape 4K UHD
chakula mezani kwake, mahali pa kukaa watumishi wake, kazi ya watumisshi wake na mavazi yao, pia wabebakikombe na mavazi yao, na namna alivyotoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Yahwe, hapakuwa na roho zaidi ndani yake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akasema kwa mfalme, “Ni kweli, taarifa ninioisikia katika nchi yangu kuhusu maneno yako na hekima yako.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Sikuamini nilichokisika mpaka nilipokuja hapa, na sasa macho yangu yamekiona. Sikuambiwa nusu kuhusu hekima yako na utajiri wako! Umeuzidi umaarufu niliokuwa nimesikia kuhusu wewe.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wamebarikiwa watu wako, na watumishi wako ambao husimama mbele yako, kwa sababu wanaisikia hekima yako. (Baadhi ya maandiko yanasema, “Wambarikiwa wake zako”, ikidhaniwa kwamba kifungu hicho kinapaswa kusomeka kama ilivyo katika Wafalme 10: 8).
Square Portrait Landscape 4K UHD
Amebarikiwa Yahwe Mungu wako, ambaye amepata raha ndani yako, aliyekuweka juu ya kiti chake cha enzi, ili uwe mfalme kwa ajili ya Yahwe Mungu wako. Kwa sababu Mungu wako inaipenda Israeli, ili kuwathibisha milele, amekufanya kuwa mfalme juu yao, ili ufanye hukumu na haki.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akampa mfalme talanta 120 za dhahabu na kiasi kikubwa manukato na vit vya thamani. Selemani hakupewa tena kiasi kikubwa cha manukato kama hiki amabacho alipewa na malakia wa Sheba.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Watumishi wa Hiramau na wa mfalme Selemani, ambaye alileta dhahabu kutoka Ofiri, miti ya msandali,, na vito vya thamani.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kwa miti hiyo ya msandali, mfalme Selemani akatengeneza madari ya nyumba ya Yahwe na nyumba yake, na vinubi na vinanda kwa ajili ya wanamziki. Hapajaonekana tena mbao kama hiyo katika nchi ya Yuda.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mfalme Selemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotaka, chochote alichoomba, zaidi ya vile alivyoleta kwa mfalme Selemani. Kwa hiyo akaondoka na kurudi kwenye nchi yake, yeye na wataumishsi wake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Sasa uzito wa dhahabu ambayo ililetwa kwa Selemani ndani ya mwaka mmoja ulikuwa talanta 666 za dhahabu,
Square Portrait Landscape 4K UHD
nje na dhahabu ambayo waliileta wachukuzi na wafanya biashara. Walme wote wa Arabuni na maliwali katika nchi pia wakamletea Selemanai dhahabu na fedha.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mfalme Selemani akatengeneza ngao kubwa mia mbili za dhahabu iliyofuliwa. Shekeli mia sita za dhahabu zikatumika kwa kila ngao.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Pia akatengeneza ngao mia tatu za shahabu iliyopigwa. Minas tatu za dhahabu zikaenda kwa kila ngao; mfalme akaziweka kwenye ikulu ya Msitu wa Lebanoni.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha mfalme atengeneza kiti cha enzi kikubwa cha pembe na kufunika kwa dhahabu safi.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kulikuwa na ngazi sita kwenda kwenye kiti cha enzi, na sehemu ya juu ya kiti cha enzi ilikuwa duara. Kulikuwa na mikono kila upande wa kiti, na simba wawili wamesimama pembeni na hiyo mikono.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Simba kumi na wawili walisimama juu ya zile ngazi, mmoja kila upande wa ngazi sita.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hapakuwa na kiti cha enzi kama hicho katika ufalme wowote mwingine. Vikombe vyote vya kunywea vya Selemani vilikuwa vya dhahabu, na vikombe vyote vya mfalme katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu halisi. Hakuna hata kimoja kilichokuwa cha fedha kwa sababu fedha haikuchuliwa kuwa ya thamani katika siku za Selemani.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mfalme alikuwa na meli zilizosafiri baharini, pamoja na meli za Hiramu. Mara moja kwa mwaka meli zilileta dhahabu, fedha, na pembe, na manukato, na pia nyani na tausi.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kwa hiyo Mfalme Selemani aliawazidi utajiri na hekima wafalme wote wa dunia.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Dunia yote waliutafuta uwepo wa Selemanai ili kusikia hekima yake, ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Waliomtembelea walileta kodi, vyombo vya shaba na dhahabu, nguo, silaha, na manukato, na farasi na anyumbu, mwaka baada ya mwaka.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Selemani alikuwa na mazizi elfu nne kwa ajili ya farasi na magari, na wapanda farasi kumi na mbili elfu, ambao waliwaweka katika miji ya magari na pamoja naye katika Yerusalemu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akatawala juu ya wafalme wote kutoka mto Efrati hadi nchi ya Wafilisti, na hadi mpaka wa Misiri.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mfalme alikuwa na fedha katika Yerusalemu, nyingi kama mawe juu ya aridhi. Akazifanya mbao za mierezi kuwa nyingi kama miti ya mikuyu ambayo iko nyanda za chini.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakaleta farasi kutoka Misri na kutoka nchi zote kwa ajili ya Selemani.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kwa mambo mengine kuhusu Selemani, mwanzo na mwisho, hayajandikwa katika Historia ya Nathani Nabii, katika unabii wa Abiya Mshinoni, na katika Maono ya Ido mwonaji wa mambo ya Yeroboamu mwana wa Nabati?
Square Portrait Landscape 4K UHD
Selemani akatawala katika Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akalala na babu zake na watu wakamzika katika mji wa Daudi baba yake. Rehoboamu, mwanaye, akawa mfalme katika sehemu yake.
Available Bible Translations
2 Chronicles 9 (ASV) »
2 Chronicles 9 (KJV) »
2 Chronicles 9 (GW) »
2 Chronicles 9 (BSB) »
2 Chronicles 9 (WEB) »
2 Chroniques 9 (LSG) »
2 Chronik 9 (LUTH1912) »
2 इतिहास 9 (HINIRV) »
2 ਇਤਿਹਾਸ 9 (PANIRV) »
2 বংশাৱলি 9 (BENIRV) »
2 நாளாகமம் 9 (TAMIRV) »
2 इतिहास 9 (MARIRV) »
2 దినవృత్తాంతాలు 9 (TELIRV) »
2 કાળવૃતાંત 9 (GUJIRV) »
2 ಪೂರ್ವಕಾಲವೃತ್ತಾಂತ 9 (KANIRV) »
٢ أخبار 9 (AVD) »
דברי הימים ב 9 (HEB) »
2 Crônicas 9 (BSL) »
2 Sử Ký 9 (VIE) »
2 Crónicas 9 (RVA) »
2 Cronache 9 (RIV) »
历 代 志 下 9 (CUVS) »
歷 代 志 下 9 (CUVT) »
2 Kronikave 9 (ALB) »
2 Krönikeboken 9 (SV1917) »
2 Паралипоменон 9 (RUSV) »
2 хроніки 9 (UKR) »
2 Krónika 9 (KAR) »
2 Летописи 9 (BULG) »
歴代志下 9 (JPN) »
2 Krønikebok 9 (NORSK) »
2 Kronik 9 (POLUBG) »
Taariikhdii Labaad 9 (SOM) »
2 Kronieken 9 (NLD) »
2 Krønikebog 9 (DA1871) »