Ufunuo 20 SWHULB
Ufunuo Chapter 20 SWHULB Bible Verse Images
Copyright © 2019 Door43 World Missions Community
Language: Kiswahili (Swahili)
Translation by: Door43 World Missions Community
Contributors: Alfred Danjuma, Bariki Malisa, Christina Abraham Kileo, Cloud Roman, Daniel Marura Chacha, Dina Mast, Dina Roman, Donald Shadarck Dutuyi, Emmanuel Masanja Mbaaga, Emmanuel Nyamalya, Erasmus Peter Malelo, Ev. Lazaro Chalomhola, Ezekiel Manala, Fred, Gabriel Gidale Merus, Gabriel Lwitakubi Mazige, James Makula, James Semnkai, Jeremiah Masasi, Jesse Katabi Masolwa, John Ojasi, Joyce Gilbert Masasi, Karen Riecks, Kazwanomo, Kennedy, Ker, Lameck Yakobo Tobotobo, Laurent Petro Malelo, Lazarus David Chalomhola, Makene Mafwele, Marco Luma Mahushi, Mathew Nkusa, Mathias William, Mr. James Semnkai .It., Musa Isaya Majama, Musa Luzali, Pastor John Kerim, Pastor Jordan, Philipo Mussa Kanwelle, Raphael Musa, Rev. Charles Mabisa, Rev. Yohana Batano, Robert Ndalahwa, Sadiki Kulwa, Samson Nungwana, Thobias Kazwanomo, Yohana Dutuyi, Yohana Magera, Zelote Loilang'akaki Lukumay, Rev. Erasmus Peter Malelo, Ev. Mathew Kazimoto, Rev. Dr. David Magoke, Rev. Elias Ndema, Rev. Alex Nyuri, Rev. Gungutu Elias, Rev. Lameck Tobotobo, Rev. Catherin D. Matia, Rev. Yohana S Dutuyi, Rev. Donald Dutuyi, GS. Andrew Gewe, Ev. Ezekiel Daudi, Rev. John Ndaluka, Ev. Moses Malugu, Rev. Moses Eliakim Ndege, Past. Isack A. Gomugo, Past. Mathias William, Rev. Yekonia M. Koko, Rev. Elisande Mhanga, Ev. James A. Makula.
This translation is made available to you under the terms of the Creative Commons Attribution Share-Alike license 4.0.
You have permission to share and redistribute this Bible translation in any format and to make reasonable revisions and adaptations of this translation, provided that:
- You include the above copyright and source information.
- If you make any changes to the text, you must indicate that you did so in a way that makes it clear that the original licensor is not necessarily endorsing your changes.
- If you redistribute this text, you must distribute your contributions under the same license as the original.
Credits: In addition, we would like to give very special thanks to eBible.org for making Swahili Unlocked Literal Bible available in MySQL format.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha niliona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa na ufunguo wa shimo lisilo na mwisho na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Alimshika yule joka, nyoka wa zamani, ambaye ni ibilisi au Shetani, na kumfunga miaka elfu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Alimtupa kwenye shimo lisilo na mwisho, akalifunga na kulitia mhuri juu yake. Hii ilikuwa hivyo ili kwamba asiwadanganye mataifa tena mpaka miaka elfu itakapoisha. Baada ya hapo, ataachiwa huru kwa muda mchache.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha niliona viti vya enzi. Waliokuwa wamevikalia ni wale ambao walikuwa wamepewa mamlaka ya kuhukumu. Vilevile niliona nafsi za wale ambao walikuwa wamekatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda kuhusu Yesu na kwa neno la Mungu. Walikuwa hawajamwabudu mnyama au sanamu yake, na walikataa kupokea alama juu ya paji za nyuso zao au mkono. Walikuja uzimani, na wakatawala pamoja na Kristo kwa miaka elfu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wafu waliobaki hawakuja uzimani mpaka miaka elfu ilipokuwa imeisha. Huu ndio ufufuo wa kwanza.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mbarikiwa na mtakatifu ni mtu yeyote ambaye achukua nafasi katika ufufuo wa kwanza! Mauti ya pili haina nguvu juu ya watu kama hawa. Patakuwa na makuhani wa Mungu na wa Kristo na watatawala na yeye kwa miaka elfu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakati miaka elfu itakapofikia mwisho, Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Atakwenda nje kuwadanganya mataifa katika kona nne za dunia -Gogu na Magogu - kuwaleta pamoja kwa ajili ya vita. Watakuwa wengi kama mchanga wa bahari.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Walikwenda juu kwenye tambarare ya nchi nao walizunguka kambi ya waumini, mji upendwao. Lakini moto ulikuja kutoka mbinguni na kuwaangamiza.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Shetani, ambaye aliwadanganya, alitupwa ndani ya ziwa liwakalo kiberiti, ambamo mnyama na nabii wa uongo walikuwa wameshatupwa. Watateswa mchana na usiku milele na milele.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha niliona kiti cha enzi kikubwa cheupe na yule ambaye alikaa juu yake. Dunia na mbingu zilikimbia mbali kutoka katika uwepo wake, lakini hapakuwako nafasi ya wao kwenda.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Niliwaona waliokufa - hodari na wasio wa muhimu wamesimama katika kiti cha enzi, na vitabu vilifunuliwa. Kisha kitabu kingine kilifunguliwa - Kitabu cha Uzima. Wafu walihukumiwa kwa kile kilichoandikwa ndani ya vitabu, matokeo ya kile walichokifanya.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Bahari iliwatoa wafu ambao walikuwa ndani yake. Kifo na kuzimu viliwatoa wafu ambao walikuwa ndani yake, na wafu walihukumiwa kulingana na walichofanya.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kifo na kuzimu zilitupwa ndani ya ziwa la moto. Hii ni mauti ya pili - ziwa la moto.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kama jina la yeyote halikupatikana limeandikwa ndani ya Kitabu cha Uzima, alitupwa ndani ya ziwa la moto.*
Available Bible Translations
Revelation 20 (ASV) »
Revelation 20 (KJV) »
Revelation 20 (GW) »
Revelation 20 (BSB) »
Revelation 20 (WEB) »
Apocalypse 20 (LSG) »
Offenbarung 20 (LUTH1912) »
प्रकाशितवाक्य 20 (HINIRV) »
ਪਰਕਾਸ਼ ਦੀ ਪੋਥੀ 20 (PANIRV) »
पপ্রত্যাদেশ 20 (BENIRV) »
வெளிப்படுத்தின விசேஷம் 20 (TAMIRV) »
प्रकटीकरण 20 (MARIRV) »
ప్రకటన గ్రంథం 20 (TELIRV) »
પ્રકટીકરણ 20 (GUJIRV) »
ಪ್ರಕಟಣೆ 20 (KANIRV) »
رُؤيا 20 (AVD) »
ההתגלות 20 (HEB) »
Apocalipse 20 (BSL) »
Khải Huyền 20 (VIE) »
Apocalipsis 20 (RVA) »
Apocalisse 20 (RIV) »
启 示 录 20 (CUVS) »
启 示 录 20 (CUVT) »
Zbulesa 20 (ALB) »
Uppenbarelseboken 20 (SV1917) »
Откровение 20 (RUSV) »
Об'явлення 20 (UKR) »
Jelenések 20 (KAR) »
Откровение 20 (BULG) »
ヨハネの黙示録 20 (JPN) »
Åpenbaringen 20 (NORSK) »
Objawienie 20 (POLUBG) »
Muujintii 20 (SOM) »
Openbaring 20 (NLD) »
Aabenbaringen 20 (DA1871) »