Marko 10 SWHULB
Marko Chapter 10 SWHULB Bible Verse Images
Copyright © 2019 Door43 World Missions Community
Language: Kiswahili (Swahili)
Translation by: Door43 World Missions Community
Contributors: Alfred Danjuma, Bariki Malisa, Christina Abraham Kileo, Cloud Roman, Daniel Marura Chacha, Dina Mast, Dina Roman, Donald Shadarck Dutuyi, Emmanuel Masanja Mbaaga, Emmanuel Nyamalya, Erasmus Peter Malelo, Ev. Lazaro Chalomhola, Ezekiel Manala, Fred, Gabriel Gidale Merus, Gabriel Lwitakubi Mazige, James Makula, James Semnkai, Jeremiah Masasi, Jesse Katabi Masolwa, John Ojasi, Joyce Gilbert Masasi, Karen Riecks, Kazwanomo, Kennedy, Ker, Lameck Yakobo Tobotobo, Laurent Petro Malelo, Lazarus David Chalomhola, Makene Mafwele, Marco Luma Mahushi, Mathew Nkusa, Mathias William, Mr. James Semnkai .It., Musa Isaya Majama, Musa Luzali, Pastor John Kerim, Pastor Jordan, Philipo Mussa Kanwelle, Raphael Musa, Rev. Charles Mabisa, Rev. Yohana Batano, Robert Ndalahwa, Sadiki Kulwa, Samson Nungwana, Thobias Kazwanomo, Yohana Dutuyi, Yohana Magera, Zelote Loilang'akaki Lukumay, Rev. Erasmus Peter Malelo, Ev. Mathew Kazimoto, Rev. Dr. David Magoke, Rev. Elias Ndema, Rev. Alex Nyuri, Rev. Gungutu Elias, Rev. Lameck Tobotobo, Rev. Catherin D. Matia, Rev. Yohana S Dutuyi, Rev. Donald Dutuyi, GS. Andrew Gewe, Ev. Ezekiel Daudi, Rev. John Ndaluka, Ev. Moses Malugu, Rev. Moses Eliakim Ndege, Past. Isack A. Gomugo, Past. Mathias William, Rev. Yekonia M. Koko, Rev. Elisande Mhanga, Ev. James A. Makula.
This translation is made available to you under the terms of the Creative Commons Attribution Share-Alike license 4.0.
You have permission to share and redistribute this Bible translation in any format and to make reasonable revisions and adaptations of this translation, provided that:
- You include the above copyright and source information.
- If you make any changes to the text, you must indicate that you did so in a way that makes it clear that the original licensor is not necessarily endorsing your changes.
- If you redistribute this text, you must distribute your contributions under the same license as the original.
Credits: In addition, we would like to give very special thanks to eBible.org for making Swahili Unlocked Literal Bible available in MySQL format.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu aliondoka eneo hilo na akaenda katika mkoa wa Uyahudi na eneo la mbele ya Mto Yorodani, na makutano walimfuata tena. Aliwafundisha tena, kama ilivyokuwa kawaida yake kufanya.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na Mafarisayo walikuja kumjaribu na wakamuuliza, “Ni halali kwa mwanamume kuachana na mke wake?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakasema, “Musa aliruhusu kuandika cheti cha kuachana na kisha kumfukuza mwanamke.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
“Ni kwa sababu ya mioyo yenu migumu ndiyo maana aliwaandikia sheria hii,” Yesu aliwaambia.
Square Portrait Landscape 4K UHD
“Lakini kutoka mwanzo wa uumbaji, 'Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke.'
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kwa sababu hii mwanamume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake,
Square Portrait Landscape 4K UHD
na hao wawili watakuwa mwili mmoja; Kwa kuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Walipokuwa ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza tena kuhusu hili.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akawaambia, “Yeyote amwachaye mke wake na kumwoa mwanamke mwingine, anafanya uzinzi dhidi yake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mwanamke naye akimwacha mme wake na kuolewa na mwanamme mwingine, anafanya uzinzi.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Nao walimletea watoto wao wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini Yesu alipotambua hilo, hakufurahishwa nalo kabisa akawaambia, “Waruhusuni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie, kwa sababu walio kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ukweli nawaambia, yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hakika hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha akawachukua watoto mikononi mwake na akawabariki akiwawekea mikono yake juu yao.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na alipoanza safari yake mtu mmoja alimkimbilia na akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu Mwema, nifanye nini ili niweze kurithi uzima ya milele?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na Yesu akasema, “Kwa nini unaniita mwema? Hakuna aliye mwema, isipokuwa Mungu peke yake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Unazijua amri: 'Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, mheshimu baba na mama yako'.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mtu yule akasema, “Mwalimu, haya yote nimeyatii tangu nikiwa kijana.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu alimwangalia na kumpenda. Akawambia, “Unapungukiwa kitu kimoja. Unapaswa kuuza vyote ulivyo navyo na uwape masikini, na utakuwa na hazina mbinguni. Ndipo uje unifuate.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini alikata tamaa kwa sababu ya maelezo haya; aliondoka akiwa mwenye huzuni, kwa kuwa alikuwa na mali nyingi.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu akatazama pande zote na kuwaambia wanafunzi wake, “Ni jinsi gani ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wanafunzi walishangazwa kwa maneno haya. Lakini Yesu akawaambia tena, “Watoto, ni jinsi gani ilivyo vigumu kuingia katika ufalme wa Mungu!
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano, kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Walishangazwa sana na wakasemezana, “Hivyo nani ataokoka”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu akawaangalia na kusema, “ Kwa binadamu haiwezekani, lakini sio kwa Mungu. Kwa kuwa katika Mungu yote yanawezekana.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
“Petro akaanza kuzungumza naye, “Angalia tumeacha vyote na tumekufuata.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu akasema, “Ukweli nawaambia ninyi, hakuna aliyeacha nyumba, au kaka, au dada, au mama, au baba, au watoto, au ardhi, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,
Square Portrait Landscape 4K UHD
ambaye hatapokea mara mia zaidi ya sasa hapa duniani: nyumba, kaka, dada, mama, watoto, na ardhi, kwa mateso, na ulimwengu ujao, uzima wa milele.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Walipokuwa njiani, kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa amewatangulia mbele yao. Wanafunzi walishangaa, na wale waliokuwa wanafuata nyuma waliogopa. Ndipo Yesu akawatoa pembeni tena wale kumi na wawili na akaanza kuwaambia ambacho kitamtokea hivi karibuni:
Square Portrait Landscape 4K UHD
“Tazama, tunakwenda mpaka Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atafikishwa kwa makuhani wakuu na waandishi. Watamhukumu afe na watamtoa kwa watu wa Mataifa.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Watamdhihaki, watamtemea mate, watampiga fimbo, na watamwua. Lakini baada ya siku tatu atafufuka.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walikuja kwake na kusema, “Mwalimu, tunakuhitaji utufanyie chochote tukuombacho.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakasema, “Turuhusu tukae nawe katika utukufu wako, mmoja katika mkono wako wa kuume na mwingine mkono wako wa kushoto.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini Yesu aliwajibu, “Hamjui mnachoomba. Mnaweza kukinywea kikombe ambacho nitakiywea au kustahimili ubatizo ambao nitabatizwa?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakamwambia, “Tunaweza” Yesu akawaambia, “Kikombe nitakachokinywea, mtakinywea. Na ubatizo ambao kwao nimebatizwa, mtaustahimili.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini atakayekaa mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto sio mimi wa kutoa, lakini ni kwa wale ambao kwao imekwisha andaliwa.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu akawaita kwake na kusema, “Mnajua kuwa wale wanaodhaniwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala, na watu wao mashuhuri huwaonyesha mamlaka juu yao.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini haipaswi kuwa hivi kati yenu. Yeyote atakaye kuwa mkubwa kati yenu lazima awatumikie,
Square Portrait Landscape 4K UHD
na yeyote atakaye kuwa wa kwanza kati yenu ni lazima awe mtumwa wa wote.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kwa kuwa Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika, na kuyatoa maisha yake kuwa fidia kwa wengi.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakaja Yeriko. Alipokuwa akiondoka Yeriko na wanafunzi wake na kundi kubwa, mwana wa Timayo, Batimayo, kipofu mwombaji, alikaa kando ya barabara.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Aliposikia kuwa ni Yesu Mnazareti, alianza kupiga kelele na kusema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wengi walimkemea yule kipofu, wakimwambia anyamaze. Lakini alilia kwa sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu alisimama na kuamuru aitwe. Walimwita yule kipofu, wakisema, “Kuwa shujaa! Inuka! Yesu anakuita.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akalitupa pembeni koti lake, akakimbia zaidi, na kuja kwa Yesu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu akamjibu na kusema, “Unataka nikufanyie nini?” Yule mwanaume kipofu akamjibu, “Mwalimu, ninataka kuona.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu akamwambia, “Nenda. Imani yako imekuponya.” Hapo hapo macho yake yakaona; na akamfuata Yesu barabarani.
Available Bible Translations
Mark 10 (ASV) »
Mark 10 (KJV) »
Mark 10 (GW) »
Mark 10 (BSB) »
Mark 10 (WEB) »
Marc 10 (LSG) »
Markus 10 (LUTH1912) »
मरकुस 10 (HINIRV) »
ਮਰਕੁਸ 10 (PANIRV) »
মার্ক 10 (BENIRV) »
மாற்கு 10 (TAMIRV) »
मार्क 10 (MARIRV) »
మార్కు 10 (TELIRV) »
માર્ક 10 (GUJIRV) »
ಮಾರ್ಕನು 10 (KANIRV) »
مَرْقُس 10 (AVD) »
הבשורה על־פי מרקוס 10 (HEB) »
Marcos 10 (BSL) »
Mác 10 (VIE) »
Marcos 10 (RVA) »
Marco 10 (RIV) »
马 可 福 音 10 (CUVS) »
馬 可 福 音 10 (CUVT) »
Marku 10 (ALB) »
Markus 10 (SV1917) »
Марка 10 (RUSV) »
Марка 10 (UKR) »
Márk 10 (KAR) »
Марко 10 (BULG) »
マルコによる福音書 10 (JPN) »
Markus 10 (NORSK) »
Marka 10 (POLUBG) »
Markos 10 (SOM) »
Markus 10 (NLD) »
Markus 10 (DA1871) »