Marko 6 SWHULB
Marko Chapter 6 SWHULB Bible Verse Images
Copyright © 2019 Door43 World Missions Community
Language: Kiswahili (Swahili)
Translation by: Door43 World Missions Community
Contributors: Alfred Danjuma, Bariki Malisa, Christina Abraham Kileo, Cloud Roman, Daniel Marura Chacha, Dina Mast, Dina Roman, Donald Shadarck Dutuyi, Emmanuel Masanja Mbaaga, Emmanuel Nyamalya, Erasmus Peter Malelo, Ev. Lazaro Chalomhola, Ezekiel Manala, Fred, Gabriel Gidale Merus, Gabriel Lwitakubi Mazige, James Makula, James Semnkai, Jeremiah Masasi, Jesse Katabi Masolwa, John Ojasi, Joyce Gilbert Masasi, Karen Riecks, Kazwanomo, Kennedy, Ker, Lameck Yakobo Tobotobo, Laurent Petro Malelo, Lazarus David Chalomhola, Makene Mafwele, Marco Luma Mahushi, Mathew Nkusa, Mathias William, Mr. James Semnkai .It., Musa Isaya Majama, Musa Luzali, Pastor John Kerim, Pastor Jordan, Philipo Mussa Kanwelle, Raphael Musa, Rev. Charles Mabisa, Rev. Yohana Batano, Robert Ndalahwa, Sadiki Kulwa, Samson Nungwana, Thobias Kazwanomo, Yohana Dutuyi, Yohana Magera, Zelote Loilang'akaki Lukumay, Rev. Erasmus Peter Malelo, Ev. Mathew Kazimoto, Rev. Dr. David Magoke, Rev. Elias Ndema, Rev. Alex Nyuri, Rev. Gungutu Elias, Rev. Lameck Tobotobo, Rev. Catherin D. Matia, Rev. Yohana S Dutuyi, Rev. Donald Dutuyi, GS. Andrew Gewe, Ev. Ezekiel Daudi, Rev. John Ndaluka, Ev. Moses Malugu, Rev. Moses Eliakim Ndege, Past. Isack A. Gomugo, Past. Mathias William, Rev. Yekonia M. Koko, Rev. Elisande Mhanga, Ev. James A. Makula.
This translation is made available to you under the terms of the Creative Commons Attribution Share-Alike license 4.0.
You have permission to share and redistribute this Bible translation in any format and to make reasonable revisions and adaptations of this translation, provided that:
- You include the above copyright and source information.
- If you make any changes to the text, you must indicate that you did so in a way that makes it clear that the original licensor is not necessarily endorsing your changes.
- If you redistribute this text, you must distribute your contributions under the same license as the original.
Credits: In addition, we would like to give very special thanks to eBible.org for making Swahili Unlocked Literal Bible available in MySQL format.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na akaondoka hapo na kwenda mjini kwao, na wanafunzi wake wakamfuata.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika Sinagogi. Watu wengi walimsikia na wakashangazwa. Wakasema, “Amepata wapi mafundisho haya?” “Ni hekima gani hii aliyopewa?” “Anatendaje miujiza hii kwa mikono yake?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
“Je huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simioni? Je dada zake si wanaishi papa hapa pamoja nasi?” Na hawakufurahishwa na Yesu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika mji wake na miongoni mwa ndugu zake na nyumbani mwake.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hakuweza kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache akawaponya.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Alishangazwa sana kwa sababu ya kutokuamini kwao. Kisha alivitembelea vijiji vya jirani akifundisha.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Aliwaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili. Aliwapa mamlaka juu ya pepo wachafu,
Square Portrait Landscape 4K UHD
na kuwaamuru wasichukue chochote wanapokwenda isipokuwa fimbo tu. Wasichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kibindoni;
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na akawaambia, “Nyumba yoyote mtakayoingia, kaeni hapo mpaka mtakapoondoka.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na mji wowote usipowapokea wala kuwasikiliza, ondokeni kwao, kung'uteni mavumbi ya miguu yenu, iwe ushuhuda kwao.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Nao wakaenda wakitangaza watu watubu na kuacha dhambi zao.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Waliwafukuza pepo wengi, na waliwapaka mafuta wagonjwa na wakaponywa.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mfalme Herode aliposikia hayo, kwa kuwa jina la Yesu lilikuwa limejulikana sana. Baadhi walisema, “Yohana mbatizaji amefufuka na kwa sababu hiyo, hii nguvu ya miujiza inafanya kazi ndani yake.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Baadhi yao wakasema, “Huyu ni Eliya,” Bado wengine wakasema, “Huyu ni nabii, kama mmoja wa wale manabii wa zamani.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini Herode aliposikia haya akasema, “Yohana, niliyemkata kichwa amefufuliwa.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Maana Herode mwenyewe aliagiza Yohana akamatwe na alimfunga gerezani kwa sababu ya Herodia (mke wa kaka yake Filipo) kwa sababu yeye alikuwa amemuoa.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kwa maana Yohana alimwambia Herode, “Si halali kumuoa mke wa kaka yako.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini Herodia alianza kumchukia na alikuwa akitaka kumuua, lakini hakuweza,
Square Portrait Landscape 4K UHD
maana Herode alimwogopa Yohana; alijua kwamba ni mwenye haki mtu mtakatifu, na alimwacha salama. Na alipoendelea kumsikiliza alihuzunika sana, lakini alifurahi kumsikiliza.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hata ilipofika wakati mwafaka ikiwa imekaribia siku ya kuzaliwa Herode akawaandalia moafisa wake karamu, na makamanda, na viongozi wa Galilaya.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ndipo binti wa Herodia akaingia na kucheza mbele yao, akamfurahisha Herode na wageni walioketi wakati wa chakula cha jioni. Ndipo mfalme akamwambia binti, “Niombe chochote unachotaka nami nitakupa.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akamwapia na kusema, chochote utakachoniomba, nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akatoka nje akamuuliza mama yake, “Niombe nini?” Akasema, “Kichwa cha Yohana Mbatizaji.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na mara moja akaingia kwa mfalme akaanza kusema, “Nataka unipatie ndani ya sahani, kichwa cha Yohana Mbatizaji.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mfalme alisikitishwa sana, lakini kwa sababu ya kiapo chake na kwa ajili ya wageni, hakuweza kumkatalia ombi lake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hivyo, mfalme akatuma askari kati ya walinzi wake na kuwaagiza kwenda kumletea kichwa cha Yohana. Mlinzi alikwenda kumkata kichwa akiwa kifungoni.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akakileta kichwa chake kwenye sahani na kumpatia binti, na binti akampa mama yake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na wanafunzi wake waliposikia hayo, walikwenda kuuchukua mwili wake wakaenda kuuzika kaburini.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na mitume, walikusanyika pamoja mbele ya Yesu, wakamweleza yote waliyofanya na waliyoyafundisha.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Naye akawaambia, “Njooni wenyewe mahali pa faragha na tupumzike kwa muda.” Watu wengi walikuwa wanakuja na kuondoka, hata hawakupata nafasi ya kula.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hivyo wakapanda mashua wakaenda mahali pa faragha peke yao.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini waliwaona wakiondoka na wengi wakawatambua, kwa pamoja walikimbia kwa miguu kutoka miji yote, nao wakafika kabla yao.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Walipofika pwani, aliona umati mkubwa na akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Na akaanza kuwafundisha mambo mengi.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Muda ulipoendelea sana, wanafunzi wakamjia wakamwambia,”Hapa ni mahali pa faragha na muda umeendelea.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Uwaage waende miji ya jirani na vijiji ili wakajinunulie chakula.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini akawajibu akisema, “Wapeni ninyi chakula.” Wakamwambia, “Tunaweza kwenda na kununua mikate yenye thamani ya dinari mia mbili na kuwapa wale?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akawambia,” Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” walipopata wakamwambia, “Mikate mitano na samaki wawili.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akawaamuru watu waketi katika makundi juu ya majani mabichi.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakawaketisha katika makundi; makundi ya mamia kwa hamsini.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha akachukua mikate mitano na samaki wawili, na kutazama mbinguni, akaibariki kisha akawapa wanafunzi waweke mbele ya umati. Na kisha aligawa samaki wawili kwa watu wote.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Walikusanya vipande vya mikate iliyobaki, Vikajaa vikapu kumi na viwili, na pia vipande vya samaki.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na walikuwa wanaume elfu tano waliokula mikate.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mara akawaambia wapande kwenye mashua waende sehemu nyingine, hadi Bethsaida, wakati Yeye akiwaaga makutano.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Walipokuwa wamekwisha kuondoka, akaenda mlimani kuomba.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kulipokuwa jioni, na mashua yao wakati huo ikiwa katikati ya bahari, naye alikuwa peke yake nchi kavu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na aliwaona wakitaabika kupiga makasia kwa sababu upepo uliwazuia. Ilipokaribia asubuhi akawaendea, akitembea juu ya maji, na alitaka kuwapita.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini walipomwona anatembea juu ya maji, wakaingiwa na wasiwasi wakidhani ni mzimu hata wakapiga kelele.
Square Portrait Landscape 4K UHD
kwa sababu walimwona wakajawa na hofu. Mara akasema nao akawaambia, “Muwe wajasiri! ni mimi! Msiwe na hofu.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akaingia ndani ya mashua, na upepo ukaacha kuvuma, nao wakamshangaa kabisa.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hivyo hawakuwa wameelewa maana ya ile mikate. Maana akili zao zilikuwa na uelewa mdogo.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Nao walipovuka ng'ambo, walifika nchi ya Genesareti mashua ikatia nanga.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakakimbia kutangaza katika mkoa mzima na wakaanza kuwaleta wagonjwa kwa machela, kila waliposikia anakuja.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Popote alipoingia katika vijiji, au mjini, au katika nchi, waliwaweka wagonjwa mahali pa soko, na wakamsihi awaruhusu kugusa pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa waliponywa.
Available Bible Translations
Mark 6 (ASV) »
Mark 6 (KJV) »
Mark 6 (GW) »
Mark 6 (BSB) »
Mark 6 (WEB) »
Marc 6 (LSG) »
Markus 6 (LUTH1912) »
मरकुस 6 (HINIRV) »
ਮਰਕੁਸ 6 (PANIRV) »
মার্ক 6 (BENIRV) »
மாற்கு 6 (TAMIRV) »
मार्क 6 (MARIRV) »
మార్కు 6 (TELIRV) »
માર્ક 6 (GUJIRV) »
ಮಾರ್ಕನು 6 (KANIRV) »
مَرْقُس 6 (AVD) »
הבשורה על־פי מרקוס 6 (HEB) »
Marcos 6 (BSL) »
Mác 6 (VIE) »
Marcos 6 (RVA) »
Marco 6 (RIV) »
马 可 福 音 6 (CUVS) »
馬 可 福 音 6 (CUVT) »
Marku 6 (ALB) »
Markus 6 (SV1917) »
Марка 6 (RUSV) »
Марка 6 (UKR) »
Márk 6 (KAR) »
Марко 6 (BULG) »
マルコによる福音書 6 (JPN) »
Markus 6 (NORSK) »
Marka 6 (POLUBG) »
Markos 6 (SOM) »
Markus 6 (NLD) »
Markus 6 (DA1871) »