Marko 15 SWHULB
Marko Chapter 15 SWHULB Bible Verse Images
Copyright © 2019 Door43 World Missions Community
Language: Kiswahili (Swahili)
Translation by: Door43 World Missions Community
Contributors: Alfred Danjuma, Bariki Malisa, Christina Abraham Kileo, Cloud Roman, Daniel Marura Chacha, Dina Mast, Dina Roman, Donald Shadarck Dutuyi, Emmanuel Masanja Mbaaga, Emmanuel Nyamalya, Erasmus Peter Malelo, Ev. Lazaro Chalomhola, Ezekiel Manala, Fred, Gabriel Gidale Merus, Gabriel Lwitakubi Mazige, James Makula, James Semnkai, Jeremiah Masasi, Jesse Katabi Masolwa, John Ojasi, Joyce Gilbert Masasi, Karen Riecks, Kazwanomo, Kennedy, Ker, Lameck Yakobo Tobotobo, Laurent Petro Malelo, Lazarus David Chalomhola, Makene Mafwele, Marco Luma Mahushi, Mathew Nkusa, Mathias William, Mr. James Semnkai .It., Musa Isaya Majama, Musa Luzali, Pastor John Kerim, Pastor Jordan, Philipo Mussa Kanwelle, Raphael Musa, Rev. Charles Mabisa, Rev. Yohana Batano, Robert Ndalahwa, Sadiki Kulwa, Samson Nungwana, Thobias Kazwanomo, Yohana Dutuyi, Yohana Magera, Zelote Loilang'akaki Lukumay, Rev. Erasmus Peter Malelo, Ev. Mathew Kazimoto, Rev. Dr. David Magoke, Rev. Elias Ndema, Rev. Alex Nyuri, Rev. Gungutu Elias, Rev. Lameck Tobotobo, Rev. Catherin D. Matia, Rev. Yohana S Dutuyi, Rev. Donald Dutuyi, GS. Andrew Gewe, Ev. Ezekiel Daudi, Rev. John Ndaluka, Ev. Moses Malugu, Rev. Moses Eliakim Ndege, Past. Isack A. Gomugo, Past. Mathias William, Rev. Yekonia M. Koko, Rev. Elisande Mhanga, Ev. James A. Makula.
This translation is made available to you under the terms of the Creative Commons Attribution Share-Alike license 4.0.
You have permission to share and redistribute this Bible translation in any format and to make reasonable revisions and adaptations of this translation, provided that:
- You include the above copyright and source information.
- If you make any changes to the text, you must indicate that you did so in a way that makes it clear that the original licensor is not necessarily endorsing your changes.
- If you redistribute this text, you must distribute your contributions under the same license as the original.
Credits: In addition, we would like to give very special thanks to eBible.org for making Swahili Unlocked Literal Bible available in MySQL format.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Asubuhi na mapema wakuu wa makuhani walikutana pamoja na wazee na waandishi na baraza zima la wazee. Kisha wakamfunga Yesu wakampeleka kwa Pilato. Pilato akamwuliza, “wewe ni Mfalme wa Wayahudi?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakuu wa makuhani wakaeleza mashitaka mengi juu ya Yesu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Pilato akamwuliza tena, “Hujibu chochote? Huoni jinsi wanavyokushtaki kwa mambo mengi?
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini Yesu hakumjibu Pilato, na hiyo ilimshangaza.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kwa kawaida wakati wa sikukuu humfungulia mfungwa mmoja, mfungwa waliyemwomba.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kulikuwapo wahalifu gerezani, miongoni mwa wauaji kati ya walioasi wanaotumikia makosa yao. Alikuwepo mtu mmoja aitwaye Baraba.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Umati ulikuja kwa Pilato, na kumwomba afanye kama alivyofanya huko nyuma.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Pilato akawajibu na kusema, “Mnataka niwafungulie Mfalme wa Wayahudi?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kwa kuwa alijua ni kwa sababu ya wivu wakuu wa makuhani walimkamata Yesu na kumleta kwake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini wakuu wa makuhani walichochea umati kupiga kelele kwa sauti kwamba afunguliwe Baraba badala yake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Pilato akawajibu tena na kusema, “Nimfanye nini Mfalme wa Wayahudi?
Square Portrait Landscape 4K UHD
Pilato akasema, “Amefanya jambo gani baya?” Lakini wakazidi kupiga kelele zaidi na zaidi “Msulibishe.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Pilato akitaka kuwaridhisha umati, akawafungulia Baraba. Akampiga Yesu mijeledi kisha akamtoa ili asulibiwe.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Askari walimwongoza hadi ndani ya ua (ule ulio ndani ya kambi) na walikusanyika pamoja kikosi cha askari.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakamvika Yesu kanzu ya rangi ya zambarau, na wakasokota taji ya miiba wakamvika.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakaanza kumdhihaki na kusema, “Salam, Mfalme wa Wayahudi!”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakampiga kichwani kwa mwanzi na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake kwa kumheshimu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua ile kanzu ya rangi ya zambarau na kumvika mavazi yake, na wakamtoa nje kwenda kumsulibisha.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakamlazimisha mpita njia kumsaidia, aliyekuwa anaingia mjini kutoka shamba. Aitwaye Simoni Mkirene (baba yake Iskanda na Rufo); wakamlazimisha kubeba msalaba wa Yesu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Askari wakampeleka Yesu mahali paitwapo Goligotha (maana ya tafsiri hii ni, Sehemu ya Fuvu la kichwa).
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakampa mvinyo iliyochanganywa na manemane, lakini hakunywa.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakamsulibisha na wakagawana mavazi yake, wakayapigia kura kuamua kipande atakachopata kila askari.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakaweka juu yake ubao ulioandikwa shitaka, “Mfalme wa Wayahudi.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Walimsubisha pamoja na majambazi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine kushoto kwake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
(Zingatia: Mstari huu, “Na maandiko yakatimia yaliyonena” haumo katika nakala za kale).
Square Portrait Landscape 4K UHD
Nao waliokuwa wakipita walimtukana, wakitikisa vichwa vyao wakisema, “Aha! wewe utakayevunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu,
Square Portrait Landscape 4K UHD
jiokoe mwenyewe na ushuke chini toka msalabani!”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kwa namna ile ile wakuu wa makuhani walimdhihaki wakisemezana, pamoja na waandishi na kusema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kristo Mfalme wa Israel, shuka chini sasa toka msalabani, ili tuweze kuona na kuamini.” Na wale waliosulubiwa pamoja naye pia walimdhihaki.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ilipofika saa sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa tisa.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakati wa saa tisa, Yesu alipiga kelele kwa sauti kubwa, “Eloi, Eloi, lama sabaktani?” ikiwa na maana “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Baadhi ya hao waliosimama waliposikia wakasema, “Tazama, anamwita Eliya.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mtu mmoja akakimbia, akajaza siki katika sponji na kuiweka juu ya mti wa mwanzi, akampa ili anywe. Mtu mmoja akasema, “Ngoja tuone kama Eliya atakuja kumshusha chini.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Pazia la hekalu likagawanyika vipande viwili toka juu mpaka chini.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ofisa mmoja aliyekuwa amesimama akimwelekea Yesu, alipoona amekufa kwa jinsi ile, akasema, “Kweli huyu mtu alikuwa Mwana wa Mungu.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Walikuwepo pia wanawake waliokuwa wakitazama kwa mbali. Miongoni mwao alikuwepo Mariamu Magdalena, Mariamu (mama yake Yakobo mdogo wa Yose), na Salome.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakati alipokuwa Galilaya walimfuata na kumtumikia. Na wanawake wengine wengi pia waliambatana naye hadi Yerusalemu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kulipokuwa jioni, na kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio, siku kabla ya Sabato,
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yusufu wa Arimathaya alikuja pale. Alikuwa ni mjumbe wa Baraza anayeheshimiwa mtu anayeutarajia Ufalme wa Mungu. Kwa ujasiri akaenda kwa Pilato, na kuuomba mwili wa Yesu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Pilato akashangazwa kwamba Yesu tayari amekufa; akamwita yule afisa akamwuliza kama Yesu amekufa.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Alipopata uhakika kwa afisa kwamba amekufa, alimruhusu Yusufu kuuchukua mwili.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yusufu alikuwa amenunua sanda. Akamshusha toka msalabani, akamfunga kwa sanda, na kumweka ndani ya kaburi lililochimbwa katika mwamba. Kisha akalivingirisha jiwe mlangoni mwa kaburi.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake Yose waliona sehemu alipozikwa Yesu.
Available Bible Translations
Mark 15 (ASV) »
Mark 15 (KJV) »
Mark 15 (GW) »
Mark 15 (BSB) »
Mark 15 (WEB) »
Marc 15 (LSG) »
Markus 15 (LUTH1912) »
मरकुस 15 (HINIRV) »
ਮਰਕੁਸ 15 (PANIRV) »
মার্ক 15 (BENIRV) »
மாற்கு 15 (TAMIRV) »
मार्क 15 (MARIRV) »
మార్కు 15 (TELIRV) »
માર્ક 15 (GUJIRV) »
ಮಾರ್ಕನು 15 (KANIRV) »
مَرْقُس 15 (AVD) »
הבשורה על־פי מרקוס 15 (HEB) »
Marcos 15 (BSL) »
Mác 15 (VIE) »
Marcos 15 (RVA) »
Marco 15 (RIV) »
马 可 福 音 15 (CUVS) »
馬 可 福 音 15 (CUVT) »
Marku 15 (ALB) »
Markus 15 (SV1917) »
Марка 15 (RUSV) »
Марка 15 (UKR) »
Márk 15 (KAR) »
Марко 15 (BULG) »
マルコによる福音書 15 (JPN) »
Markus 15 (NORSK) »
Marka 15 (POLUBG) »
Markos 15 (SOM) »
Markus 15 (NLD) »
Markus 15 (DA1871) »